1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ndege sita za tornado zapelekwa Afghanistan

2 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCD3

Ndege sita aina ya tornado zimeondoka leo kwenda Afghanistan kusaidia vikosi vya jeshi la ISAF linaloongozwa na shirika la kujihami la kambi ya magharibi, NATO.

Akizungumza wakati wa sherehe ya kuondoka kwa ndege hizo waziri wa ulinzi wa Ujerumani, Franz Josef Jung, amesema ndege hizo zitaliimarisha jeshi la ISAF na kuboresha operesheni za usalama.

Kiongozi wa chama cha SPD hapa Ujerumani, Kurt Beck, amesema Ujerumani kufikia sasa imefanya kazi kwa njia ya sawa na ni muhimu imefanya hivyo.

´Tunachokifanya kufikia sasa kwa hakika ni muhimu. Sifutilii mbali uwezekano wetu kwamba tutarefusha mamlaka ya kuziruhusu ndege hizo kukaa zaidi Afghanistan. Na bila shaka sio kwamba tunachukua majukumu mapya bali kutimiza kikamilifu majukumu tuliyo nayo kwa wakati huu.´

Ndege za torando zinatarajiwa kuwasili katika kambi ya jeshi la Ujerumani huko Mazar i Sharif kufikia mwishoni mwa wiki hii.