1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Mwenyekiti wa SPD asema hatagombea wadhfa wake katika uongozi ujao

1 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEMs

Juhudi za kuafikia mapatano ya kuunda serikali ya mseto nchini Ujerumani zimetibuka baada ya mwenyekiti wa chama cha SPD Franz Müntefering kutangaza uamuzi wa wake wa ghafla kuwa hatagombea wadhfa wake katika uchaguzi ujao.

Bwana Münterfering ametoa uamuzi huo mara tu chama chake cha SPD kilipokiuka pingamizi yake na kumteua mwanaharakati kijana wa mlengo wa kushoto kuchukua nafasi ya katibu mkuu wa chama cha SPD.

Bwana Franz Münterfering alitazamiwa kuchukua wadhfa wa makamu wa kansela na waziri wa kazi katika serikali ya mseto wa vyama vya CDU/CSU na SPD.

Haijulikani iwapo uamuzi wake huo utaathiri uteuzi wake.

Kansela mteule bibi Angela Merkel amesema mazungumzo ya serikali ya mseto yanatarajiwa kukamilika Novemba 12.