BERLIN: Mwanamke wa kijerumani ataka mwananawe aachiliwe huru
11 Julai 2007Mwanamke wa kijerumani aliyeachiliwa huru nchini Irak, Hanelore Krause, amewataka watekaji nyara wanaomzuilia mwananwe wa kiume, Sinan, wamuachilie huru.
Hapo awali waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani, Frank Walter Steinmeier, alitangaza kuachiliwa huru kwa mwanamke huyo aliyetekwa nyara nchini Irak mapema mwaka huu. Aidha waziri Steinmeier alisema Hannelore Krause mwenye umri wa miaka 61 sasa yuko katika ubalozi wa Ujerumani mjini Baghdad.
´Kuzuiliwa kwa Bi Hannelore Krause kwa siku 155 kumemalizika. Tangu jana yuko huru na yuko chini ya ulinzi wa Ujerumani katika ubalizo wetu mjini Baghdad.´
Hata hivyo Frank Walter Steinmeier alisema mtoto wa kiume wa mama huyo, Sinan, bado anazuiliwa na watekaji nyara lakini akaahidi serikali itaendelea kufanya kila inaloweza kumuokoa kijana huyo.
Hannelore Krause na mwanawe, Sinan, walitekwa nyara mnamo tarehe 6 Februari mwaka huu nchini Irak.