BERLIN : Mtambo wa nuklea wa Ujerumani wafungwa
22 Julai 2007Mtambo wa nuklea wa Ujerumani ambao ulifungwa mwezi uliopita na kusababisha kushutumiwa kwa kampuni inayouendesha mtambo huo ya Sweden shughuli zake zimesimamishwa kwa muda usiojulikana kwa ajili ya kufanyiwa ukaguzi zaidi wa usalama.
Maafisa wanasema wataalamu wa masuala ya usalama wa nuklea wamegunduwa kushindwa kufanya kazi kwenye mfumo wa dharura wa kupooza mtambo huo ulioko kwenye mji wa Brunsbüttel katika mkoa wa kaskazini wa Schleswig-Holstein. Mtambo huo ulikatishwa na mtandao mkuu wa umeme baada ya kupasha moto kupindukia hapo tarehe 28 Juni juu ya kwamba uliendelea kuzalisha umeme kwa matumizi yake yenyewe.
Masaa kadhaa baada ya tukio hilo moto ulizuka kwenye mtambo wa nuklea ulioko karibu na hapo wa Krummel ambao unamilikiwa na kampuni hiyo hiyo ya Vattental.
Maafisa wa serikali ya Ujerumani wameishutumu kampuni hiyo kwa kushindwa kurepoti ukubwa hasa wa matatizo katika mitambo yake.