1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Mshukiwa wa pili akamatwa nchini Lebanon

24 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDIM

Mshukiwa wa pili wa njama ya mashambulio ya mabomu ndani ya treni hapa nchini Ujerumani mwezi uliopita, amekamatwa hii leo nchini Lebanon.

Kwa mujibu wa ofisi ya muongoza mashtaka mkuu wa serikali ya Ujerumani mjini Berlin, mtuhumiwa huyo alijiwasilisha mwenyewe kwa maofisa wa polisi mjini Tripoli nchini Lebanon. Polisi sasa wanatafuta njia ya kumrejesha mwanamume huyo hapa nchini.

Polisi wa mjini Kiel kaskazini mwa Ujerumani walimtia mbaroni mshukiwa mwingine, raia wa Lebanon mwenye umri wa miaka 21, Jumamosi iliyopita.

Mtuhumiwa huyo amekuwa akizuiliwa kwa mashtaka ya kujaribu kuua na kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi.

Wanaume wote wawili wanashtakiwa kwa kutega mabomu yaliyopatikana ndani ya treni mnamo Julai 31 mjini Dortmund na Koblenz.

Mabomu yote mawaili yalifeli kulipuka kwa makosa yaliyofanywa na watuhumiwa hao wakati wa kuyatega.