BERLIN: Msaada zaidi kutoa mafunzo ya kijeshi
7 Julai 2007Matangazo
Waziri wa masuala ya nje wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier anataka kupeleka Afghanistan, maafisa zaidi wanaotoa mafunzo ya kijeshi. Amesema,polisi na majeshi ya Afghanistan yapaswa kusaidiwa mpaka yatakapoweza kusimamia usalama na utaratibu peke yake.