1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Mkuu wa Siemens ashinikizwa kujiuzulu

7 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCBz

Mkuu wa bodi ya usimamizi ya kampuni ya Siemens ya Ujerumani Heinrich von Peirer yuko katika shinikizo la kutakiwa ajiuzulu kutokana na madai ya rushwa.

Kwa mujibu wa gazeti la kila wiki nchini Ujerumani la Spiegel wajumbe kadhaa kwenye bodi hiyo na chama cha wafanyakazi cha IG Metal wanataka von Pieter ajiuzulu kwa madai ya kuwapa fedha kinyume cha sheria chama cha wafanyakazi wa kituo kinachounga mkono msimamo wa kibiashara wa kampuni hiyo wakati alipokuwa mtendaji mkuu wa kampuni ya Siemens.

Bodi hiyo huenda ikadai kupatiwa orodha kamili ya malipo yaliotolewa kwa Wilheim Schelsky muasisi wa chama cha wafanyakazi cha AUB wakati wa mkutano wake ujao uliopangwa kufanyika hapo tarehe 25 mwezi huu wa April.