1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin: Mkuu wa shirika la umoja wa mataifa la usafi wa mazingira,

9 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFl2
mjerumani Klaus Töpfer amekosoa vikali "mitindo iliyofurutu" inayoshuhudiwa katika tajiri.Katika mahojiano na gazeti la "Neuen Osnabrücker Zeitung" bwana Klaus Töpfer amezungumzia juu ya " hujuma dhidi ya mazingira" zinazosababisha madhara makubwa kwa jamii na kwa ulimwengu kwa jumla.Amesema sio jambo linaloingia akilini kwamba mafukara walipe sehemu ya gharama za neema ya matajiri .Bwana Klaus Töpfer amesisitiza shehena ya kutosha ya maji ni muhimu katika juhudi za kuimarisha amani katika nchi zinazoinukia.Amesema shirika la umoja wa mataifa la usafi wa mazingira linashughulikia pia juhudi za kupambana na kuchafuliwa mazingira kulikosababishwa na na vita,katika eneo la Balkan,Afghanistan na hivi sasa nchini Iraq.