Berlin: Mkuu wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa ataka kuweko kodi ya ziyada kwa tiketi za ndege
18 Februari 2007Matangazo
Kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, mkurugenzi wa Shirika la Ulinzi wa Mazingira la Umoja wa Mataifa, Aachim Steiner, ametaka kuweko kodi ziyada kwa tiketi za ndege. Aliliambia gazeti la BILD am Sonntag la hapa Ujerumani kwamba kufanya hivyo msafiri anayekwenda likizo hatokuwa na fikra potofu kwamba safari ya ya kwenda Mallorca inagharimu Euro 19 tu. Bwana Steiner alisema pia bei ya mafuta ni rahisi mno. Wakati huo huo alionya juu ya matokeo mabaya ya dunia kuwa na ujoto zaidi jambo litakalosababisha kuweko wakimbizi wa hali ya hewa. Kupanda juu kwa maji ya bahari kwa nusu mita tu kunaweza kupelekea, kwa mfano, kwa watu milioni 30 katika Bangladesh wasiwe na mahala tena pa kuishi.