BERLIN: Mkutano wa Uislamu kuweka msingi wa maelewano
27 Septemba 2006Matangazo
Nchini Ujerumani viongozi wa serikali wamekutana na wajumbe 15 wa jumuiya ya waislamu.Hii ni mara ya kwanza kwa viongozi wa serikali kujadili hofu za kundi hilo la wachache ambalo ni asili mia 4 ya umma nchini Ujerumani.Mkutano uliofanywa katika kasri la Charlottenburg mjini Berlin ni mwanzo wa majadiliano yatakayofanywa kati ya serikali na viongozi wa kiislamu kwa kipindi cha miaka miwili hadi mitatu ijayo.Azma ni kuweka msingi mpya wa majadiliano hayo.Waziri wa ndani wa Ujerumani,Wolfgang Schäuble alieufungua mkutano huo amesema,majadiliano yalikuwa ya wazi na kuridhisha.Kiasi ya waislamu milioni 3.2 huishi nchini Ujerumani na kuna kama mashirika 70 ya kiislamu.