BERLIN: Mkutano wa tatu kati ya SPD na CDU
5 Oktoba 2005
Wakuu wa chama cha Social Democrats cha Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani hii leo wanakutana na chama cha Christian Democrtas cha Angela Merkel katika duru ya tatu ya majadiliano ya kuunda serikali ya muungano.Vyama hivyo vinabishana juu ya suala nani atakaekuwa kansela mpya wa Ujerumani.Kiongozi wa chama cha SPD -Franz Münterfering amesema Schröder lazima abakie kama kansela kwa awamu ya tatu.Kwa wakati huo huo chama cha Merkel cha CDU kinasema chama chake kina mamlaka ya kuingoza serikali mpya kwa sababu vyama vya kihafidhina vya CDU na CSU kwa pamoja vimeshinda viti vinne zaidi ya SPD katika uchaguzi uliofanywa mwezi uliyopita.Maafisa wa CDU pia wamesema kuwa chama cha SPD lazima kikubali sharti hilo kabla ya kuanzishwa rasmi mazungumzo yo yote kuhusu serikali ya mseto.