1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Mkutano wa NATO wajadili hali ya shirika hilo huko Afghanistan.

14 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEb8

Maafisa wakuu wa shirika la kujihami la mataifa ya magharibi NATO wanakutana mjini Berlin kujaribu kuepusha hali ya kutokukubaliana juu ya hali ya baadaye ya shirika hilo huko Afghanistan.

Siku nne kabla ya uchaguzi muhimu wa bunge nchini Afghanistan , waziri wa ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld amezungumzia uwezekano wa kupunguza majeshi ya Marekani nchini humo.

Amesema kuwa muda umefika kwa mataifa wanachama wa NATO kusaidia kupambana na wapiganaji wa chini kwa chini wa Taliban. Uingereza inaunga mkono wito wa Rumsfeld kwa majeshi yanayoongozwa na NATO kuchukua nafasi ya mapambano zaidi nchini humo. Lakini mataifa mengine wanachama , ikiwa ni pamoja na Ujerumani na Ufaransa zimekataa mpango utaipa NATO nafasi ya juu katika kazi za kulinda amani na kupambana na waasi.