1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Mkutano wa mzozo wa nuklea wa Iran waahirishwa

16 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7FU

Mkutano wa mataifa makubwa juu ya mzozo wa nuklea wa Iran umeahirishwa katika kile kinachoonekana kama ni kutofurahishwa kwa China juu ya ziara iliopewa hadhi kubwa ya Dalai Lama nchini Marekani.

Mkutano huo wa hapo kesho wa maafisa waandamizi kutoka nchi tano wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Ujerumani mjini Berlin umeahirishwa hadi wiki ijayo.

Dalai Lama anatarajiwa kutunukiwa Medali ya Dhahabu ya Bunge ambapo Rais George W. Bush anatazamiwa kuhudhuria sherehe za kutunukiwa medali hiyo.