1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa NATO

14 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEbQ

Mkutano wa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi-NATO hii leo utahusika na masuala muhimu ya kijeshi kama vile mchango wake nchini Afghanistan.Wakati wa mkutano huo wa mawaziri wa ulinzi,ulioanza siku ya jumanne mjini Berlin, ilidhihirika kuwa pendekezo la Marekani la kutaka kujumuisha vikosi vya Nato ISAF pamoja na vikosi vya kupambana na ugaidi vya Marekani,hivi sasa haliwezi kutekelezwa.Waziri wa ulinzi wa Ujerumani,Peter Struck amesema utaratibu wa kuwa na kile alichokieleza “nguzo mbili chini ya paa moja” utaendelea.Hata waziri wa ulinzi wa Ufaransa Michele Alliot-Marie amesema,ushirikiano unaweza kuboreshwa,lakini opresheni za kila kundi ziendelee kutengwa.Masuala mengine yaliokuwemo katika ajenda ya mkutano huo wa siku mbili mjini Berlin,ni huduma za NATO huko Kosovo na katika jimbo la Darfur nchini Sudan na pia msaada wa kutoa mafunzo kwa jeshi la Iraq.