1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Mkufunzi atimuliwa jeshini

17 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9C

Jeshi la Ujerumani Bundeswher limemtimuwa mkufunzi aliyechukuliwa filamu wakati akimuamuru kuruta kufikiria kama anamtwanga risasi za bunduki ya rashasha Mmarekani mweusi wakati wa mazoezi.

Afisa huyo wa jeshi atapoteza cheo chake na masalio ya mshahara na marupurupu.Askari aliechukuwa filamu hiyo yuko chini ya uchunguzi.

Tukio hilo limetokea mwezi wa Julai mwaka jana katika msitu karibu na kambi ya jeshi katika mji wa kaskazini wa Rendsbug.

Jeshi la Ujerumani limekuwa likiandamwa na kashfa katika miezi ya karibuni.

Wakufunzi 18 wa kijeshi wanakabiliwa na mashtaka hivi sasa kwa tuhuma za kuwatendea vibaya makuruta wakati wa mafunzo hapo mwaka 2004 na mwaka jana kulijitokeza picha za wanajeshi wa Ujerumani wakiwa na mabufuru ya binaadamu wakati wakitumika nchini Afghanistan.