1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Mkataba mpya wakubaliwa na viongozi wa Umoja wa Ulaya

20 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7EK

Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel amesema, mkataba wa marekebisho uliokubaliwa na viongozi wa Umoja wa Ulaya mjini Lisbon,Ureno uidhinishwe rasmi kwa haraka.Ni matumaini yake kuwa mwakani katika majira ya joto,mkataba huo utakuwa tayari umeshaidhinishwa na mabunge ya nchi wanachama ili uanze kutumiwa mapema mwaka 2009.

Kansela Merkel amesema,Ulaya itaweza kufanya kazi vizuri zaidi.Mikoa,umma na hata mabunge ya taifa yataweza kutoa mchango.Vile vile kutakuwepo ugawaji dhahiri wa mamlaka.

Akaongezea kuwa mkataba huo mpya,utarahisisha utaratibu wa kupitisha maamuzi katika Umoja wa Ulaya.