1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Mgomo wa treni watibua huduma

27 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7CS

Huduma za treni nchini Ujerumani zimerudi kwenye hali ya kawaida baada ya mgomo wa masaa 30 wa madereva wa treni kutimua usafiri wa abiria na huduma za treni za mikoa katika sehemu kubwa ya nchi.

Chama cha wafanyakazi madereva wa treni cha GDL wameitisha mgomo huo kuashinikiza madai yake ya nyongeza ya asilimia 30 ya mishahara.Shirika la reli la taifa limekubali nyongeza ya asilimia 10 na malipo ya euro 2,000 kwa mkupuo mmoja ili madereva hao wafanye kazi kwa masaa mengi zaidi kwa wiki.

Chama cha wafanyakazi madereva wa treni kimetishia kuitisha migomo zaidi wiki ijayo venginevyo shirika la reli la Deutsche Bahn linaboresha madai yao ifikapo Jumatatu.

Shirika la Deutsche Bahn limekataa madai hayo.