1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Mgomo wa madereva wa treni waendelea

9 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C78s

Nchini Ujerumani,mgomo wa madereva wa treni ulioanza Alkhamisi mchana,unaendelea bila ya kuwepo ishara ya maafikiano.Safari hii,mgomo huo unahusika na treni za kusafirisha mizigo.

Kwa mujibu wa shirika la treni la Ujerumani, Deutsche Bahn,hadi jana jioni kama treni 300 ziliathirika lakini idadi hiyo imetazamiwa kuongezeka kwa sababu treni nyingi za mizigo husafiri wakati wa usiku.Mgomo huo utaendelea hadi Jumamosi asubuhi.Chama cha wafanyakazi madereva wa treni GDL kinadai nyongeza ya mshahara ya asilimia 30.