BERLIN: Mgomo wa madereva wa treni umemalizika
13 Oktoba 2007Matangazo
Mgomo wa siku moja uliofanywa na madereva wa treni nchini Ujerumani na kuchelewesha mamilioni ya wasafiri umemalizika.Madereva hao wamesema,mgomo umefanikiwa kwa sababu asilimia 85 ya misafara ya treni ilipaswa kufutwa.Lakini shirika la usafiri wa treni la Ujerumani “Deutsche Bahn” limesema,ni theluthi moja tu ya safari za karibu na mikoani zilizoathirika.Madereva wanadai kuongezwa mishahara kwa asilimia 30.Siku ya Jumatatu,Deutsche Bahn itatoa pendekezo jipya la nyongeza ya mishahara.