BERLIN : Merkel na Sarkozy kuzungumzia Umoja wa Ulaya
10 Septemba 2007Matangazo
Sera ya viwanda ya Ufaransa,machafuko ya masoko ya fedha na mustakbali wa Umoja wa Ulaya yatakuwa juu kwenye agenda wakati Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa watakapukutana leo katika mkutano usio rasmi mjini Berlin
Mkutano huo utakaofanyika katika kasri la Meseberg kaskazini mwa Berlin utahudhuriwa pia na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo Frank Walter Steinmeir wa Ujerumani na mwenzake wa Ufaransa Bernard Kouchner.
Mbali na suala la machafuko katika masoko ya hisa ya kimataifa msemaji wa serikali ya Ujerumani Thomas Stieg amesema Merkel na Sarkozy pia watajadili hali katika Mashariki ya Kati na Afghanistan.Suala jengine litakalokuwemo kwenye agenda ni hatima ya Kosovo.
Mwishoni mwa juma mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wameshindwa kukubaliana wakati wa mkutano wao nchini Ureno juu ya sera ya pamoja kwa mustakbali wa jimbo hilo la Serbia