1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Merkel na Kaczynski wajadili masuala ya utata

13 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7GE

Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel na Rais wa Poland,Lech Kaczynski wamekutana Berlin,siku chache kabla ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya,utakaofanywa Lisbon nchini Ureno.Viongozi hao wawili wamekutana kufuatia ombi la Poland.Kwa mara nyingine tena,wamejadili masuala ya utata kuhusu marekebisho yanayodaiwa na Poland katika mswada wa mkataba unaotazamiwa kuchukua nafasi ya Katiba ya Ulaya.Miaka miwili iliyopita katiba mpya iliyopendekezwa,ilikataliwa katika kura ya maoni iliyopigwa nchini Ufaransa na Uholanzi. Merkel na Kaczynski wamesema,wana matumaini kuwa maafikiano yatapatikana katika mkutano wa Lisbon.