BERLIN: Merkel na Chirac wajadili hali ya Lebanon
1 Agosti 2006Matangazo
Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel amezungumza kwa simu na rais wa Ufaransa,Jacques Chirac juu ya hali ya Mashariki ya Kati.Ofisi ya msemaji wa serikali imesema,Merkel na Chirac wameeleza wasi wasi wao mkubwa kuhusu hali ya hivi sasa, inayosababisha hasara kubwa ya maisha ya watu wasio na hatia pande zote mbili.Viongozi wote wawili wamesema,makubaliano ya kudumu ya kusitisha mapigano,lazima yapatikane upesi iwezekanavyo.