BERLIN: Merkel kuzuru Mashariki ya Kati
30 Machi 2007Matangazo
Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel ataondoka kesho kuanza ziara yake ya siku tatu ya Mashariki ya Kati. Ziara yake itajumulisha mazungumzo na rais wa mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, mjini Ramallah. Bi Merkel atakutana pia na waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert mjini Jerusalem.
Ziara hiyo inafanyika kufuatia mkutano wa viongozi wa kiarabu mjini Riyadh, Saudi Arabia, ambapo mpango mpya wa amani ya Mashariki ya Kati ulifufuliwa. Mkutano huo uliitaka Israel iukabali mpango huo.