BERLIN : Merkel kukutana na Putin
17 Mei 2007Kansela Angela Merkel wa Ujerumani anatazamiwa kuelekea katika mji wa kusini wa Urusi wa Samara kukutana na Rais Vladimir Putin siku moja kabla ya mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya na Urusi kwenye mji huo.
Merkel anatazamiwa kukutana na Putin na Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso akiwa katika wadhifa wake kama rais wa Umoja wa Ulaya.Mkutano huo wa viongozi unakuja huku kukiwa na ongezeko la mvutano kati ya Umoja wa Ulaya na Urusi juu ya masuala mbali mbali.
Mojawapo ya masuala hayo ikiwa ni kupiga marufuku kwa Urusi kuagizia nyama kutoka Poland na Estonia kuhamisha alama ya kumbukumbu ya vita ya enzi ya muungano wa Urusi kutoka katika eneo la mji mkuu wake wa Tallinn.
Urusi pia inapinga mpango wa Umoja wa Mataifa unaoungwa mkono na Umoja wa Ulaya wa kuipatia jimbo la Kosovo uhuru utakaokuwa chini ya usimamizi wa kimataifa.