1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Merkel kuitembelea Poland

16 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCIS

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel atafanya ziara rasmi ya siku mbili nchini Poland. Lengo la ziara hiyo ni kuboresha uhusiano baina ya nchi hizo mbili.

Mazungumzo yanatarajiwa kutuwama juu ya tofauti zilizopo baina ya Ujerumani na Poland kuhusu katiba ya Umoja wa Ulaya, ambayo kansela Merkel ameapa kuifufua kama rais wa umoja huo.

Mpango wa Marekani kutaka kuweka vituo vya kuzuia mashambulio ya maroketi mashariki mwa Ulaya pia utajadiliwa. Merkel anailaumu Poland kwa kuruhusu makombora ya Marekani kuwekwa nchini humo bila kuidhinishwa na shirika la NATO.

Wakati wa ziara yake kansela Merkel amepangiwa kukutana na waziri mkuu wa Poland, Jaroslaw Kaczynski na kakake Lech Kaczynski, ambaye ni rais wa nchi hiyo.