BERLIN: Merkel hana mpango wa kuwatuma wanajeshi wa Ujerumani kwenda Lebanon
30 Julai 2006Matangazo
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, ameliambia gazeti moja hapa nchini kwamba hana wazo la kuwatuma wanajeshi wa Ujerumani kushiriki katika kikosi cha kimataifa kitakachopelekwa kwenda Lebanon.
Merkel amesema mpaka sasa bado hakuna mamlaka ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Ameongeza kwa kusema uwezo wa Ujerumani kutekeleza operesehni za kijeshi katika mataifa ya kigeni unafikia ukingoni.
Wakati huo huo, waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani, Wolfgang Schauble, amesema ni mapema mno kupendekeza kuwaruhusu wakimbizi wa Lebanon waingine Ujerumani.