BERLIN : Merkel azungumza na Abbas na Olmert
14 Juni 2007Matangazo
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amezungumzia ongezeko la wimbi la umwagaji damu wa Gaza na Rais Mahamoud Abbas wa Palestina halikadhalika Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert.
Merkel amerudia tena kuunga mkono juhudi za kutafuta amani za Rais wa Palestina wakati wa mazungumzo yake hayo kwa njia ya simu.
Maafisa mjini Berlin wamesema Olmert pia ameelezea kuwa tayari kwake kuendelea kushirikiana na Abbas.