1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Merkel atunukiwa tuzo ya Kiyahudi

1 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTw

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amechaguliwa kutunukiwa tuzo ya Wayahudi wa Kijerumani inayojulikana kwa jina la Leo Baeck.

Baraza kuu la Wayahudi nchini Ujerumani limemteuwa Merkel kutokana na kujizatiti kwake kujenga upya uhusiano kati ya Wayahudi na watu wasio Wayahudi halikadhalika kati ya Ujerumani na Israel.

Kansela Merkel ambaye wiki hii alitangazwa kuwa mwanamke mkakamavu kabisa nambari moja duniani na gazeti la Marekani la Forbes atapokea tuzo hiyo katika hafla itakayofanyika mjini Berlin hapo tarehe sita mwezi wa Septemba.