1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Merkel asifu mpango mpya wa kujumuisha jamii za wageni

13 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBjC

Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel amesifu mpango mpya wa taifa wa kujumuisha wageni katika jamii za Kijerumani,kama ni hatua iliyo muhimu. Alipozungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari,baada ya kukutana na viongozi wa makabila mbali mbali mjini Berlin,aliutangaza mpango wa serikali kusaidia jamii za walio wachache.Sehemu ya mpango huo mpya ni kutoa mafunzo zaidi ya lugha ya Kijerumani ili kuweza kuwajumuisha wageni,bora zaidi katika jamii za Kijerumani.