BERLIN: Merkel amualika Brown kutembelea Ujerumani
29 Juni 2007Matangazo
Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel amemualika waziri mkuu wa Uingereza,Gordon Brown kuitembelea Ujerumani atakapokuwa na nafasi ya kwanza kufanya hivyo.Kansela Merkel anatumaini kuwa chini ya uongozi wa Brown,serikali za Uingereza na Ujerumani zitaendelea kuwa na uhusiano wa karibu. Amesema,hilo hasa ni muhimu kwa Ulaya na uhusiano mzuri pamoja na Marekani.