Berlin. Merkel amshutumu mwanachama mwenzake kwa kumsifu jaji wa enzi za Nazi.
14 Aprili 2007Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amemtupia lawama mwanachama mwandamizi wa chama chake cha Christian Democratic kwa kutetea sifa mbaya ya jaji wa kijeshi wa zamani wa chama cha Nazi.
Akizungumza katika mazishi ya Hans Filbinger, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 93, waziri mkuu wa jimbo la baden –Württemberg Günther Oettinger amesema kuwa Filbinger alikuwa ni mpinzani wa utawala wa Nazi, lakini hakuwa na uwezo wa kuukimbia.
Merkel amesema katika taarifa kuwa ingekuwa bora Oettinger angetumia hotuba hiyo kujadili masuala muhimu yanayohusiana na enzi za utawala wa Nazi.
Filbinger alikuwa waziri mkuu wa jimbo la Baden-Württemberg kuanzia mwaka 1966 hadi 1978 hadi alipojiuzulu baada ya kugundulika kuwa aliwahukumu watu akiwa kama jaji wa jeshi la majini wakati wa enzi za utawala wa Manazi.