BERLIN: Merkel amekutana na Topolanek kutafuta maafikiano
17 Juni 2007Matangazo
Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel hii leo amekutana na Waziri mkuu Mirek Topolanek wa Jamhuri ya Czech,karibu na mji wa Berlin.Mkutano huo ni sehemu ya juhudi zake za kutafuta maafikiano kuhusika na mkataba wa katiba ya Umoja wa Ulaya uliokwama.Ni matumaini ya Merkel kuwa masikilizano yatapatikana,kabla ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya,utakaofanywa mjini Brussels siku ya Alkhamisi na ya Ijumaa.Kansela Merkel siku ya Jumamosi alikutana pia na Rais Lech Kaczynski wa Poland lakini viongozi hao hawakuweza kuafikiana.Mgogoro unahusika na dai la Poland la kutaka mfumo wa kupiga kura katika umoja huo ubadilishwe kwa manufaa ya madola madogo na ya wastani.