1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Merkel aitaka Uturuki kuvumilia dini nyengine

23 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC7t

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ameitaka Uturuki kuchukuwa hatua kuonyesha kwamba ni taifa linalovumulia Ukristo.

Kauli yake hiyo inakuja kufuatia kuuwawa kwa Wakristo watatu akiwemo Mjerumani mmoja katika mji wa kusini wa Uturuki wa Malatya wiki iliopita.

Merkel amesema katika mahojiano ya toleo la leo la gazeti la Ujerumani kwamba mauaji hayo ni kielelezo cha kutokukubalika kwa uvumilivu. Watu hao watatu wawili wakiwa ni Waturuki waliobadili dini na kuingia Ukristo walikutikana wakiwa wamekufa baada ya kuchinjwa kwenye nyumba ya kuchapisha Biblia Jumatano iliopita.

Hata hivyo Merkel ambaye nchi yake inashikilia urais wa kupokezana wa Umoja wa Ulaya amesema kwamba tukio hilo halitoathiri mazungumzo ya Uturuki kujiunga na Umoja wa Ulaya.