BERLIN: Mbunge wa chama cha CDU apinga Marekani kuiuzia silaha Saudi Arabia
30 Julai 2007Matangazo
Mbunge wa chama cha Christian Democratic hapa Ujerumani, Ruprecht Polenz, ameikosoa mipango ya Marekani kuiuzia silaha Saudi Arabia na nchi nyengine za Mashariki ya Kati.
Kwenye mahojiano yake na gazeti la Frankfurter Rundschau, mwenyekiti huyo wa kamati ya bunge la Ujerumani inayoshughulikia sera za kigeni, ametaka badala yake juhudi zifanywe kukusanya silaha katika eneo hilo.
Mpango wa Marekani kuuza silaha zake Mashariki ya Kati unaonekana kuwa mkakati wa kutaka kuidhibiti Iran huku nchi hiyo ikiendelea kujiimarisha.