1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin: Mazungumzo yameendelea usiku kucha kati ya kansela Gerhard Schröder na viongozi

15 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFsK
wa upande wa upinzani kuhusu mageuzi katika sera za kodi ya mapato na ajira.Hakuna maendeleo lakini yaliyopatikana."Ikilazimika tutaendelea mpaka kesho" amesema hayo mjumbe wa chama cha Social Democratioc Wilhelm Schmidt.Pande hizi mbili,serikali na upande wa upinzani zina muda wa hadi kesho jumanne kufikia makubaliano.Baadae itakua zamu ya wabunge kuyaidhinisha.Makubaliano yanapewa umuhímu mkubwa kwa ukuaji wa kiuchumi wa Ujerumani na pia kwa mustakabal wa kisiasa wa kansela Gerhard Schröder.Kansela Gerhard Schröder alisema hapo awali yuko tayari kuregeza kamba ikiwa upande wa upinzani utafanya vivyo hivyo.