BERLIN : Mawaziri wa ulinzi wa NATO wakutana Berlin
13 Septemba 2005Matangazo
Mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO wanakutana nchini Ujerumani kwa mazungumzo yasio rasmi yenye lengo la kuifanya miundo ya umoja huo kuwa ya kisasa.
Mawaziri kutoka nchi wanachama 26 watajadili namna ya kuipa uwezo NATO kupiga vita ugaidi na kuweza kukabiliana kwa haraka na hali za dharura za kimataifa.
Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Peter Struck amesema serikali yake pia inataka kuona dhima kubwa ya kisiasa kwa ajili ya NATO katika kipindi cha usoni.
Kujihusisha kwa NATO nchini Afghanistana ni mada ilioko juu kwenye agenda ya mkutano huo wa Berlin.