1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Mawaziri wa ndani wazungumzia usalama

8 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBRy

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Wolfgang Schäuble na mawaziri wenzake wa mambo ya ndani wa mikoa 16 ya Ujerumani wamekutana mjini Berlin kujadili suala la usalama kufuatia kufichuliwa kwa njama za mashambulizi ya kigaidi wiki hii.

Wamekubaliana kwamba kushiriki katika mafunzo kwenye kambi za kigaidi za kigeni na ushawishi wa kushiriki kwenye harakati za kigaidi kutafanywa kuwa sio halali nchini Ujerumani.

Schäuble ambaye ni waziri kwenye serikali ya mseto ya chama cha Cristian Demokratic cha Angela Merkel anaunga mkono uchunguzi wa kidigitali kwa watuhumiwa wa ugaidi lakini wenzake wa chama cha Social Demokatik wana mashaka na jambo hilo.

Schäuble anasema magaidi wanafaidika kutokana na mabadiliko ya haraka ya kiufundi na maafisa wa usalama nao hawana budi kuambatana na mazingira hayo halikadhalika sheria za msingi za nchi na kwa hiyo inabidi wafanye kazi zaidi.

Wajerumani wawili na Mturuki mmoja walikamatwa hapo Jumanne kwa tuhuma za kupanga njama za kushambulia vituo vya Marekani nchini Ujerumani.

Polisi bado ingali inawasaka watuhumiwa wengine saba katika njama hiyo.