1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani na Poland, kukutana juu ya katiba mpya-

15 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFj2

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Ufaransa na Poland, wanatarajiwa kukutana kesho ijumaa, kwa ajili ya kuzungumzia tena swali la katiba mpya ya jumuia ya umoja wa ulaya.

Jana, Waziri wa mambo ya kigeni wa Poland Bwana Wlodzimierz Cimoszewics, amekutana na mwenzie wa Ujerumani Joskher Fisher.

Baada ya mazungumzo yao viongozi hao wawili wamekiri bado pande mbili hazijapa kuelewana, kuhusu jinsi ya kupigia kura maamuzi muhimu, katika Jumuia ya Umoja wa ulaya itakayokuwa na wanachama ishirini na watano.

Mwishoni mwa mwaka uliopita, viongozi wakuu wa nchi za Jumuia ya Ulaya, walishindwa kuafikiana kuhusu katiba mpya ya jumuia hiyo, kutokana na mzozo uliozuka baina ya nchi kubwa zilizoanzisha jumuia hio, na nchi ndogo zilizokubaliwa uwanachama hivi karibuni, kuhusu jinsi ya kupigia kura maamuzi muhimu katika jumuia ya Umoja wa ulaya. Ikiwa hakutapatikana muafaka, inatazamiwa kuwa Jumuia ya Umoja wa ulaya itakumbana na hali ya mgawanyiko baina ya nchi kubwa kwa upande mmoja, ambazo ni Ujerumani na Ufaransa, na nchi ndogo kwa upande mwingine, ambazo nyingi ni za eneo la ulaya ya mashariki.