BERLIN: Matumaini kuhusu hatima ya Kosovo
9 Novemba 2007Matangazo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier ana matumaini kuwa kutapatikana ufumbuzi kuhusu hatima ya jimbo la Serbia la Kosovo.Mjini Berlin,alipokutana na ujumbe wa Wakosovo wenye asili ya Kialbania,waziri Steinmeier alisema,maafikiano kati ya Umoja wa Ulaya,Marekani na Urussi huenda yakapatikana ifikapo Desemba 10.Madola hayo,licha ya upinzani wa Serbia,yanaunga mkono kutoa uhuru kwa jimbo la Kosovo.