1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Mateka wa Ujerumani asihi asaidiwe

24 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBWa

Maafisa wa wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani hivi sasa wanauchunguza ukanda mpya wa video wenye kumuonyesha mwanaume wa Kijerumani anaeshikiliwa mateka na wanamgambo wanaotuhumiwa kuwa wa Taliban nchini Afghanistan.

Ukanda huo uliopatikana kutoka kwa kituo cha televisheni cha Afghanistan unamuonyesha mhandisi huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 62 ambaye ana matatizo ya moyo akiwa amedhoofu.

Katika ukanda huo amesihi kusaidiwa na kusema kwamba Taliban watamuuwa iwapo madai yao hayatotimizwa.

Mjerumani huyo alitekwa nyara kusini magharibi mwa Kabul wiki tano zilizopita lakini mahala halisi anakoshikiliwa hakujulikani.