BERLIN: Matamshi ya waziri wa ulinzi yakosolewa
17 Septemba 2007Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung anazidi kukosolewa baada ya kutoa matamshi kwamba Ujerumani haitosita kuitungua ndege ya abiria iwapo ndege hiyo itakuwa imetekwa nyara kwa ajili ya kutekeleza shambulio la kigaidi.
Mtalaamu wa maswala ya ulinzi wa chama cha SPD kilichomo kwenye serikali ya mseto Rainer Arnold amesema kwamba kuangusha ndege ya biria wasio na hatia ni hatua isiyoweza kuhalalika kikatiba.
Bwana Peter Struck kiongozi wa wabunge wa chama cha SPD amekumbusha uamuzi wa mahakama kuu ya katiba nchini Ujerumani unaotaja kwamba ndege ya abiria inaweza tu kuangushwa iwapo itakuwa imewabeba watekaji nyara peke yake na wala sio abiria wasio na hatia.
Hoja ya waziri wa ulinzi Franz Josef Jung imekosolewa pia na mwenyekiti wa cha SPD Kurt Beck na wanachama wa vyama vya kiriberali, walinzi wa mazingira na wa mrengo wa shoto Die Linke.