BERLIN: Marufuku kuvuta kwenye vyombo vya usafiri wa umma
1 Septemba 2007Matangazo
Kuanzia hii leo nchini Ujerumani ni marufuku kuvuta sigara katika vyombo vya usafiri vya umma na majengo ya serikali kuu.Wasiofuata sheria,watakabiliwa na faini ya hadi Euro 1,000.Vile vile umri wa kuweza kuvuta hadharani na kununua sigara umeongezwa kuwa miaka 18 badala ya 16.
Hata hivyo,sheria ya Ujerumani inawaruhusu wavutaji katika stesheni kubwa,kutumia sehemu au vyumba maalum vilivyowekwa kwa ajili yao.