1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin: Malalamiko ya Chama cha SPD dhidi ya Rais wa Ujerumani

9 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF5K

Kiongozi wa chama cha SPD cha hapa Ujerumani, Franz Münterfering, amewaomba wenzake chamani kuacha kumshambulia Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani. Katika mahojiano alisema kufanya hivyo sio sawa. Wakati huo alikataa kwamba yeye amepoteza kidogo mamlaka katika chama chake cha SPD.

Kutokla ofisi ya Rais inasemakana zilivuja habari juu ya mazungumzo ya siri baina ya Rais Köhler na Kansela Schroader. Inasemakana kwamba Kansela Schroader alitaja sababu ya nia yake ya kuitishwa uchaguzi mpya kwamba anhofia kubinywa na wabunge wa SPD wa mrengo wa kushoto baada ya chama cha CDU kupata ushindi katika uchauzi wa mkoa wa North Rhein Westfalia.