BERLIN: Majeshi ya Ujerumani hayatopelekwa Chad
18 Julai 2007Matangazo
Ujerumani haitoshiriki katika tume ya vikosi vya Umoja wa Ulaya,pindi kutaundwa ujumbe wa aina hiyo kuwalinda wakimbizi nchini Chad.Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel alitamka hayo kujibu taarifa ya Ufaransa ya kuweka vikosi tayari kwa ujumbe wa nchini Chad.Kiasi ya watu 250,000 kutoka Darfur wamekimbilia Chad inayopakana na jimbo la mgogoro la Sudan,Darfur.Merkel ameeleza kuwa Ujerumani inasaidia vikosi vya amani vya Umoja wa Afrika katika Darfur na hata tume ya Umoja wa Mataifa kusini mwa Sudan.