BERLIN: Maiti ya mateka wa Kijerumani yapatikana
22 Julai 2007Matangazo
Hakuna habari mpya kuhusika na utekaji nyara wa wahandisi wawili wa Kijerumani nchini Afghanistan.Hayo ni kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier. Amesema,mateka mmoja amefariki na inaelekea kuwa kifo chake kimetokana na taabu za mazingira aliyokuwa akizuiliwa.Akaongezea kuwa serikali inafanya iwezavyo kuokoa maisha ya mateka wa pili.
Wakati huo huo,waziri wa mambo ya nje wa Afghanistan,Rangin Dadfar Spanta amelaani utekaji nyara huo kwa kusema kuwa hicho ni kitendo cha unyama.Amesema,watu wa Afghanistan,wanasikia uchungu na wapo pamoja na familia za mahabusu.
Habari zingine zinasema kuwa polisi wa Afghanistan wamepata maiti ya mateka wa Kijerumani.