BERLIN : Mahkama yatafakari uchunguzi wa mawasiliano
10 Oktoba 2007Matangazo
Mahkama Kuu nchini Ujerumani inatazamiwa kuanza kusikiliza hoja kwa kiasi gani taifa linaweza kurekodi mazungumzo ya simu na kuchunguza mawasiliano ya mtandao katika juhudi za kuzuwiya ugaidi.
Suala linalojadiliwa ni sheria katika mkoa wa North Rhine Westphalia ambayo inaruhusu polisi kufanya upekuzi wa mtandao bila ya vibali vya upekuzi.
Watetezi wa suala la faragha nchini Ujerumani wanapinga hatua hizo kwa kusema kwamba ni kinyume na katiba kwa kuwa kutapelekea kupelelezwa kwa watu wa kawai