1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Madereva wa treni kugoma Ijumaa

11 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ge

Chama cha wafanyakazi madereva wa treni nchini Ujerumani GDL kimesema kitafanya mgomo wa siku nzima kwa huduma za treni za mikoa hapo kesho wakati mzozo wake wa miezi kadhaa na kampuni ya reli ya Deutsche Bahn ukiendelea.

Chama hicho cha GDL ambacho kinawakilisha madereva 34,000 kinasema madereva wake wa treni wanalipwa mishahara midogo kwa kulinganisha na wenzao walioko barani Ulaya.

Chama hicho kimekataa makubaliano yaliofikiwa kati ya shirika la reli la taifa Deutsche Bahn na vyama vyengine viwili vikubwa vya wafanyakazi kwa ongezeko la mishahara la asilimia 4.5 na kimekuwa kikitaka makubaliano tafauti ya ongezeko la mishahara la hadi asimilia 31.