1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Madereva wa reli wagoma tena

10 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBkF

Madereva wa treni nchini Ujerumani leo wamesababisha tena sehemu za usafiri wa reli nchini kushindwa kufanya kazi kutokana na mzozo wa nyongeza ya mishahara lakini uamuzi wa mahkama kuzuwiya kufanyika kwa migomo zaidi ya vyama vyao vya wafanyakazi umefupisha muda wa mgomo.

Chama cha wafanyakazi wa madereva wa GDL kinadai nyongeza ya mishahara ya hadi asilimia 31 kwa baadhi ya wanachama wake na makubaliano tafauti ya mishahara kwa madereva wake na shirika la reli la Deutsche Bahn AG.

Mgomo wao leo hii ambao ulifuatiwa na mgomo kama huo wiki iliopita umesitisha usafiri wa treni mjini Hamburg,Munich, Frankfurt na Kölon miongoni mwa miji mengine.

Mahkama ya wilaya mjni Dusseldorf imetowa hukumu kwamba mgomo huo sio halali.

Hapo jana vyama vyengine viwili vya wafanyakazi ambavyo vinawakilisha wafanyakazi tafauti wa reli vilifikia makubaliano na shirika la Deutsche Bahn ambayo wanachama wao watapatiwa ongezeko la mshahara la asilimia 4.5 hapo Januari Mosi na malipo ya mara moja ya euro 600 kwa ajili ya kipindi cha miezi sita cha pili cha mwaka huu.