BERLIN : Madaktari waandamana kuhusu kazi na malipo
6 Agosti 2005Matangazo
Zaidi ya madaktari 3,000 wa Ujerumani wenye hasira kutokana na masharti ya kazi na malipo wamekuwa na maandamano mjini Berlin.
Maandamano hayo ya jana yamekamilisha juma zima la maandamano yenye kuonyesha kuwepo kwa matatizo katika sekta ya huduma za afya kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa tarehe 18 mwezi wa Septemba. Msemaji wa shirikisho la madaktari Marbuger Bund amesema madaktari hupoteza euro bilioni moja kila mwaka zikiwa kama ni malipo yasiyolipwa ya masaa ya kazi ya ziada.
Mikoa ya Ujerumani inayokabiliwa na ukata wa fedha iko katika shinikizo linaloongezeka kupunguza gharama za matumizi ambapo wafanyakazi wa sekta ya kuhudumia umma kama vile madaktari wakiwa ndio walengwa wakuu.