BERLIN: Mabomu ya kutegwa ardhini yameua zaidi ya 5,750
12 Novemba 2007Matangazo
Kote duniani,zaidi ya watu 5,750 ama waliua au walijeruhiwa kwa mabomu yaliyotegwa chini ya ardhi.Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya mwaka ya ICBL-shirika linalofanya kampeni kupiga marufuku kutumia mabomu ya aina hiyo.
Idadi ya watu walioathirika imeongezeka katika nchi kama Pakistan,Burma, Somalia na Lebanon.Asilimia 34 ya wale waliouawa au kujeruhiwa ni watoto.